Chakutumaini sina
Sina wema wa kutosha, dhambi zangu kuziosha
Kwake Yesu nasimama, ndiye Mwamba ni salama
Ndiye Mwamba ni salama, ndiye Mwamba ni salama
Damu yake na sadaka, nategemea daima
Yote chini yakiisha, Mwokozi atanitosha.
Kwake Yesu nasimama, ndiye Mwamba ni salama
Ndiye Mwamba ni salama, ndiye Mwamba ni salama
Njia yangu iwe ndefu, Yeye hunipa wokovu
Mawimbi yakinipiga, nguvu zake ndiyo nanga
Kwake Yesu nasimama, ndiye Mwamba ni salama
Ndiye Mwamba ni salama, ndiye Mwamba ni salama
Nikiitwa hukumuni, rohoni nina amani
Nikivikwa haki yake, sina hofu mbele yake

No comments: